Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 11:10

Mahakama Kuu ya Marekani yabadili sheria ya kuruhusu utoaji mimba, Roe V Wade


Waungaji mkono haki ya utoaji mimba na wanaopinga wakusanyika nje ya Mahakama Kuu baada ya majaji kubadili sheria ya utoaji mimba Marekani
Waungaji mkono haki ya utoaji mimba na wanaopinga wakusanyika nje ya Mahakama Kuu baada ya majaji kubadili sheria ya utoaji mimba Marekani

Mahakama Kuu ya Marekani siku ya Ijumaa imetupilia mbali sheria inayoruhusu wanawake kua na haki ya haki kutoa mimba iliyopitishwa miaka 50 iliyopita.

Kwenye hatua ambayo ilikuwa imesubiriwa kwa makini , mahakama hiyo imetupilia mbali uamuzi wa nusu karne uliotoa haki ya kikatiba ya kutoa mimba na kwa hivyo sasa majimbo yameachiwa uhuru wa kuamua iwapo yataendelea na sheria hiyo au la.

Rais Joe Biden amekosoa vikali uwamuzi huo, akisema Mahakama Kuu imechukua msimamo mkali sana kupiga marufuku haki ya utoaji mimba.

"Hii ni utekelezaji wa itikadi kali na kosa lenye athari kubwa lililofanya na Mahakama Kuu kwa maoni yangu," amesema rais Biden.

Rais Biden ametoa wito kwa wamarekani kuandamana kwa amani kupinga uwamjuzi huo na kuwataka kujitokeza katika uchaguzi kuwabadili wabunge watakaoleta mabadiliko.

Tayari waungaji mkono utoaji mimba na wanaopinga wamekusanyika nje ya jengo la Mahakama Kuu ambalo liko chjini ya ulinzi mkali kupinga au kusherehekea uwamuzi huo.

Uamuzi wa mahakama hiyo yenye wahafidhina wengi, umetolewa chini ya miezi miwili baada ya nakala ya uamuzi huo kupatikana kwa siri kupitia mtandao na kuzua maandamano makubwa ya kitaifa kutoka kwa wanaharakati wa haki za utoaji mimba.

Ingawa hatua hiyo ya kubatilisha uamuzi wa 1973 maarufu kama Roe v Wade pamoja na kesi tofauti uliojulikana kama Planned Parenthood v Casey haijapiga marufuku utoaji mimba moja kwa moja, bali kuyaachia majimbo uwamuzi wao wenyewe.

Hivi sasa ni juu ya bunge kupitisha mswada ambao utafanya utowaji mimba kua sheria ya nchi, lakini tatizo ni kwamba wademokrats wanaounga mkono suala hilo hawana kura 60 kwenye Baraza la Senate kuweza kupitisha mswada kama huo.

XS
SM
MD
LG