Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 04, 2025 Local time: 06:04

Mahakama ya juu nchini Kenya  yasimamisha uamuzi wa mahakama ya chini kuhusu sheria ya fedha ya mwaka  2023


Jaji Mkuu wa Mahakama ya Juu ya Kenya Martha Koome alipohudhuria hafla ya kuapishwa kwa rais wa Kenya William Ruto, katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi, Kenya Jumanne, Septemba 13, 2022.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Juu ya Kenya Martha Koome alipohudhuria hafla ya kuapishwa kwa rais wa Kenya William Ruto, katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi, Kenya Jumanne, Septemba 13, 2022.

Mahakama ya juu nchini Kenya  siku ya Jumanne ilisimamisha uamuzi wa mahakama ya chini kwamba sheria ya fedha ya mwaka  2023 ilikuwa kinyume cha katiba, ikisema ni muhimu kulinda uthabiti katika bajeti hadi  rufaa ya serikali isikilizwe mwezi ujao.

Miswada ya fedha inayowasilishwa bungeni kila mwanzoni mwa mwaka wa fedha ndiyo chombo kikuu cha serikali kuweka bayana hatua zake za kuongeza mapato ikiwa ni pamoja na kupandisha kodi.

Uamuzi wa Mahakama ya Rufaa mwishoni mwa mwezi uliopita kwamba Sheria ya Fedha ya mwaka jana ilikuwa kinyume na katiba lilikuwa pigo kwa serikali ya Rais William Ruto, ambaye aliuondoa mswada wa fedha wa mwaka huu mwezi Juni kutokana na maandamano yaliyoongozwa na vijana, changamoto kubwa zaidi katika utawala wake wa miaka ya urais.

Forum

XS
SM
MD
LG