Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 30, 2024 Local time: 02:47

Mahakama ya Guinea kutoa hukumu ya Camara Julai 31


Mahakama ya Guinea inayosikiliza kesi ya dikteta wa zamani Moussa Dadis Camara na wengine kuhusu mauaji ya mwaka 2019, Jumatano imesema itatoa uamuzi wake Julai 31.

Pamoja na maafisa wengine 11 wa serikali na jeshi, Dadis Camara anashtakiwa kwa mauaji, unyanyasaji wa kijinsia, utesaji, ushikiliaji wa watu na utekaji nyara.

Septemba 28, 2009, na siku zilizofuata, maafisa wa ulinzi wa rais, wanajeshi, polisi na wanamgambo waliukandamiza kikatili mkutano wa upinzani kwenye uwanja wa michezo katika viunga vya mji mkuu Conakry.

Takriban watu 156 waliuwawa, wanawake 109 walibakwa na mamia ya watu walijeruhiwa, kwa mujibu wa tume ya uchunguzi iliyopewa mamlaka na Umoja wa Mataifa.

Takwimu halisi zina aminika kuwa za juu zaidi ya hizi.

Jumatano hakimu mfawidhi alitangaza tarehe ya uamuzi baada ya upande wa mashtaka na upande wa utetezi kumaliza kujieleza.

Forum

XS
SM
MD
LG