Kesi hiyo ilisikilizwa mwaka jana katika mahakama hiyo baada ya Super League kushindwa kuzinduliwa mwezi Aprili 2021. Rais wa UEFA Aleksander Ceferin aliwaita viongozi wa klabu hiyo nyoka na waongo na kutishia kuwapiga marufuku wachezaji kwenye klabu za Super League.
Kundi hilo lililoundwa na vilabu 12 vilivyoasi ambavyo sasa vinaongozwa na Real Madrid na Barcelona pekee baada ya Juventus kujiondoa mwaka huu walichukua hatua za kisheria kulinda nafasi yao na Mahakama ya Haki iliombwa kutoa uamuzi juu ya pointi za kisheria za EU na mahakama ya Madrid.
Vilabu hivyo vilishutumu UEFA kwa kukiuka sheria za Ulaya kwa madai ya kutumia vibaya utawala wake wa soko katika mashindano ya soka.
Forum