Kesi hiyo iliwasilishwa na mwanaharakati wa Namibia Friedel Dausab kwa msaada wa shirika lisilo la kiserikali lenye makao yake makuu nchini Uingereza Human Dignity Trust.
Dausab aliliambia shirika la habari la Reuters baada ya uamuzi huo wa mahakama kuwa alikuwa na furaha. Ni siku nzuri kwa Namibia alisema. Haitakuwa kosa tena kupenda.
Wanaharakati wa haki wanasema kwamba wakati hukumu chini ya sheria juu ya ulawiti na makosa yasiyo ya asili ya ngono ilikuwa nadra sana, wameendeleza ubaguzi dhidi ya jamii ya watu wa mapeni ya jinsia moja -LGBTQ na kuwafanya mashoga kuishi kwa hofu ya kukamatwa.
Forum