Mahakama ya juu Marekani leo Ijumaa inatarajiwa kusikiliza hoja za maneno dhidi ya sera mbili za utawala wa Rais Joe Biden za chanjo ya COVID-19 zilizotolewa na mashirika ya serikali ili kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya Corona unaosababisha vifo.
Sera ni muhimu kwa taifa letu katika kujibu COVID-19 msemaji wa White House, Jen Psaki alisema katika taarifa. Mamlaka yaliyotolewa yalifanyiwa tathmini na utawala wa usalama na afya kazini na vituo vya huduma kwa Medicare na Medicaid. Sera ya OSHA inawataka waajiri walio na wafanyakazi 100 au zaidi kuhakikisha kuwa wafanyakazi wao wamepewa chanjo kamili au kupimwa kila wiki.
Mamlaka ya CMS kwa wafanyakazi katika vituo vya huduma za afya wanaokubali fedha za serikali kwa Medicare na Medicaid vinawataka wafanyakazi wapewe chanjo kamili bila misamaha ikijumuisha Imani za kidini.