Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 17:21

Mahakama Cairo yamhukumu mwanaharakati kifungo jela miezi sita


Hisham Kassem, mchapishaji wa zamani wa magazeti na mwanaharakati wa kisiasa, akizungumza wakati wa mahojiano na Reuters TV, huko Cairo, Misri, Juni 13, 2023. REUTERS/Ahmed Fahmy.
Hisham Kassem, mchapishaji wa zamani wa magazeti na mwanaharakati wa kisiasa, akizungumza wakati wa mahojiano na Reuters TV, huko Cairo, Misri, Juni 13, 2023. REUTERS/Ahmed Fahmy.

 Kassem alipatikana na hatia ya kuharibu sifa za waziri wa zamani na kuwatukana maafisa katika kituo cha polisi baada ya kukamatwa alisema wakili wake, Nasser Amin.

Mahakama moja mjini Cairo siku ya Jumamosi ilimhukumu mchapishaji na mwanaharakati mashuhuri Hisham Kassem, ambaye hivi karibuni alizidisha ukosoaji wake dhidi ya utawala wa Rais Abdel Fattah al-Sisi, kifungo cha miezi sita jela, wakili wake alisema.

Kassem ni kiongozi wa kundi kipya cha kiliberali al-Tayar al-Hurr, au Free Current, ambalo limetoa wito wa kufanyika mabadiliko ya kisiasa ili kukabiliana na mzozo wa kiuchumi na kusema kuwa kinaweza kusimamisha mgombea katika uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika mapema mwaka wa 2024.

Hakuna upinzani mkali unaotarajiwa kuwepo dhidi ya Sisi, mkuu wa zamani wa jeshi ambaye ameendelea kuungwa mkono na vikosi vya usalama.

Kassem alipatikana na hatia ya kuharibu sifa za waziri wa zamani na kuwatukana maafisa katika kituo cha polisi baada ya kukamatwa alisema wakili wake, Nasser Amin. Mahakama ya masuala ya kiuchumi iliyotoa uamuzi huo pia ilimtoza faini ya paundi 20,000 za Misri.

Kesi yake ya kukata rufaa imepangwa kusikilizwa Oktoba 7, Amin alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG