Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 15:17

Maguruneti yarushwa karibu na Ikulu ya rais Somalia


Mlipuko wa gari huko Somalia.Mei 11.2022. (AP Foto/Farah Abdi Warsameh).
Mlipuko wa gari huko Somalia.Mei 11.2022. (AP Foto/Farah Abdi Warsameh).

Maguruneti yalishambulia vitongoji vya makazi karibu na ikulu ya rais katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu siku ya Jumapili muda mfupi baada ya bunge kuidhinisha baraza la mawaziri lililoteuliwa hivi karibuni nchini humo, na kusisitiza changamoto za usalama zinazoikabili serikali mpya.

Mbali na janga la njaa, taifa hilo la Pembe ya Afrika pia linakabiliwa na uasi mkubwa wa Kiislamu, huku wanamgambo wa Al-Shabaab wakizidisha mashambulizi yao katika miezi ya hivi karibuni.

Siku ya Jumapili, wakati bunge lilipokutana kuidhinisha baraza la mawaziri la Waziri Mkuu Hamza Abdi Barre lenye mawaziri 75, ambalo linamjumuisha naibu kiongozi wa zamani wa Al-Shabaab, mfululizo wa makombora yametua karibu na ikulu ya rais, kulingana na afisa wa usalama na shahidi.

XS
SM
MD
LG