Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:36

Magufuli aagiza Benki Kuu Tanzania kudhibiti fedha


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ameagiza Benki Kuu (BoT) Jumatano kudhibiti mzunguko wa fedha na kuchukua hatua za haraka dhidi ya benki ambazo hazifanyi vizuri katika juhudi ya kuzuia jinai za kifedha na kuilinda shilingi ya Tanzania.

Hatua hiyo imekuja wakati Shirika la Fedha Duniani (IMF) imeitaka Tanzania kuongeza kasi ya mabadiliko na kufanya matumizi zaidi ili kuzuia kuzorota kwa moja ya uchumi unaokua kwa kasi duniani.

Magufuli aliahidi kufanya mabadiliko katika uchumi unaochechemea kutokana na ukiritimba na kuanza programu ya kuendeleza miundo mbinu baada ya kuchaguliwa kuwa rais 2015.

“Hivi sasa tuna mabenki 58 nchini Tanzania, BoT ni lazima ifuatilie kwa karibu mabenki na kuchukua hatua za haraka dhidi ya taasisi ambazo hazifanyi vizuri. Ni bora tuwe na benki chache ambazo zinafanya vizuri kuliko kuwa na idadi kubwa ya mabenki ambayo hayana mafanikio,” amesema katika tamko lililotolewa na ofisi yake.

“Pia nataka kuwepo udhibiti wa matumizi ya dola za Marekani. Hivi ninavyoongea, dola milioni 1 zilikamatwa… uwanja wa ndege wa Dar es Salaam na hakuna maelezo kuhusu mzunguko wa pesa hizo zikiingia nchini. Ni lazima tuwe waangalifu.”

Magufuli amesema serikali yake inachukua hatua kadhaa za sera za fedha kuboresha kukopeshwa kwa sekta binafsi, na hili tayari limeonyesha unafuu wa shinikizo la kukosekana shilingi katika soko.

IMF imesema baadae Jumanne kuwa sekta ya benki Tanzania bado ipo na mitaji ya kutosha, lakini ziko benki ndogo na za kati ambazo zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa viwango vya mitaji.

Imesema kuwa kupiga hatua kumepungua, wakati kuna ukosefu wa matumizi ya serikali – ikihusisha malalamiko ya sekta binafsi kukosekana kwa sera isiyotabirika—ambayo inaathiri uchumi wa nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG