Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 30, 2024 Local time: 11:22

Magaidi 37 wameuawa Syria


Wanajeshi wa Marekani wakishika doria juu ya mfumo wa kulinda ndege dhidi ya msahambulizi kaskazini mwa Syria April 5 2024
Wanajeshi wa Marekani wakishika doria juu ya mfumo wa kulinda ndege dhidi ya msahambulizi kaskazini mwa Syria April 5 2024

Jeshi la Marekani limesema kwamba wapiganaji 37 wenye uhusiano na kundi la kigaidi la Islamic state na al-Qaeda, wameuawa katika mashambulizi mawili ya angani nchini Syria.

Wawili kati ya wapiganaji waliouwa walikuwa maafisa wa ngazi ya juu wa kundi hilo la wapiganaji.

Jeshi la Marekani limesema kwamba lilitekeleza mashambulizi hayo kaskazini mwa Syria jumanne, yaliyolenga maafisa wa ngazi ya juu wa kundi la kigaidi la Hurras al-Deen, lenye uhusiano na kundi la al-Qaeda, na makundi mengine nane.

Wametangaza pia shambulizi jingine la Septemba 16, la kiwangi kikubwa, dhidi ya kambi za kundi la kigaidi la IS katika sehemu ya kijijini katikati mwa Syria, na ambalo liliua wapiganaji 28 wakiwemo viongozi wao wanne wa Syria.

Kuna karibu wanajeshi 900 wa Marekani nchini Syria wanaojaribu kuzuia kundi la kigaidi la Islami state kujiimarisha. Kundi hilo lilikuwa limedhibithi sehemu kubwa ya Iraq na Syria mwaka 2014.

Forum

XS
SM
MD
LG