Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 08:25

Maelfu ya waandamanaji wajitokeza Austria kupinga chama cha FPO


Kiongozi wa chama cha FPO cha Austria, Herbert Kickl akihutubia wafuasi wake kufuatia matokeo ya kura mjini Vienna.
Kiongozi wa chama cha FPO cha Austria, Herbert Kickl akihutubia wafuasi wake kufuatia matokeo ya kura mjini Vienna.

Maelfu ya waandamanji Alhamisi wamekusanyika kwenye mji mkuu wa Austria, Vienna, kupinga uwezekano wa kurejea madarakani kwa chama cha mrengo wa kulia cha Freedom, FPO, kilicho ongoza kwenye uchaguzi wa kitaifa wa Jumapili.

FPO kilipata karibu asilimia 29 ya kura hiyo, kikiwa mbele ya kile cha Conservative People’s Party, kilichopata zaidi kidogo ya asilimia 26. Rihab Toumi mwanafunzi wa umri wa miaka 24 alisema kuwa,” FPO ni hatari kwa kuwa tayari kimesema kuwa kitatawala kwa sera za Viktor Orban, ambaye ni kiongozi wa nchi jirani ya Hungary.

Ingawa chama hicho kiliongoza kwenye kura, hakina uhakika kuwa kiongozi wake Herbert Kickl, mwenye misimamo mikali atapata nafasi ya kuunda serikali, kwa kuwa hakuna chama kingine cha kisiasa kilichopo tayari kushirikiana naye.

Viongozi wa maandamano walisema kuwa kati ya watu 15,000 na 17,000 walikusanyika katikati ya Vienna, na kisha kuandamana wakielekea kwenye makao ya bunge. Baadhi yao walibeba mabango yenye maneno, “Tulinde demokrasia,” Hakuna kushirikiana na rafiki wa Putin,” pamoja na mengine yenye kukashifu chama cha FPO.

Forum

XS
SM
MD
LG