Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 05:36

Maelfu ya vijana wanasajiliwa katika jeshi kupambana na waasi DRC


Wanajeshi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wakiwa karibu na mpaka wa DRC na Rwandabaada ya mapigano kuanza kuanza mashariki mwa Congo June 12, 2014.
Wanajeshi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wakiwa karibu na mpaka wa DRC na Rwandabaada ya mapigano kuanza kuanza mashariki mwa Congo June 12, 2014.

Mapigano makali yameendelea kati ya wanajeshi wa serikali na kundi la waasi la M23 masshariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, siku moja baada ya maelfu ya watu kukimbilia nchini Uganda kutoka sehemu ambazo zinashikiliwa na waasi kutokana na mashambulizi makali ya mabomu.

Wakaazi wa sehemu hiyo wameripoti milipuko mikubwa ya mabomu yanayorushwa na wanajeshi wa serikali dhidi ya waasi wa kundi la M23.

Ndege za kivita zimekuwa zikipaa mjini Goma, ambapo jeshi la serikali limeimarisha usalama kutokana na ripoti kwamba waasi wa M23 wanalenga kudhibithi mji huo muhimu wa kibiashara.

Maafisa wa usalama wamekuwa wakipiga doria katika mji wa Goma tangu jumapili usiku na kusajili vijana wanaojiunga na jeshi kwa ajili ya kupambana na waasi.

Waasi wa M23 wanaendelea kushikilia mji wa Bunagana, ulio kilomita 59 kutoka Goma. Waasi hao vile vile wanashikilia sehemu zingine ikiwemo Kiwanja, mji ulio kwenye barabara ya kutoka Bunagana hadi Goma.

Waasi wa M23, wakiongozwa na Bosco Ntaganda na Sultani Makenga, walidhibiti Goma mwaka 2012, baada ya wanajeshi wa serikali kukimbia na kuuwacha. Waasi hao waliondoka kufuatia shutuma za jumuiya ya kimataifa.

Jumla ya raia wa DRC 16,000 wamekimbilia Uganda kufuatia mapigano kati ya M23 na wanajeshi wa serikali ya DRC.

XS
SM
MD
LG