Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:06

Maelfu waandamana Ureno kupinga uhamiaji haramu


Picha ya maktaba ya waandamanaji mjini Lisbon, Ureno. Aprili 2023. (Foto: REUTERS/Pedro Nunes)
Picha ya maktaba ya waandamanaji mjini Lisbon, Ureno. Aprili 2023. (Foto: REUTERS/Pedro Nunes)

Maelfu ya waandamanaji wakipeperusha bendera ya Ureno na kuimba wimbo wa taifa walikusanyika mjini Lisbon Jumapili kuonyesha ghadhabu yao kwa  uhamiaji haramu na usiodhibitiwa

.Waandamanaji walibeba mabango wakitaka kumalizwa kwa uhamiaji mkubwa, kufukuzwa nchini kwa wahamiaji wasio na nyaraka halali. Maandamano hayo yaliitishwa na chama cha upinzani cha Chega chenye msimo wa mrengo wa kulia, ambacho ni cha tatu kwa ukubwa nchini humo.

Mbunge wa chama hicho Rui Afonso, amesema Ureno pamoja na mataifa mengine ya Ulaya yameshindwa kudhibiti wimbi la wahamiaji, hali inayozua wasi wasi wa ukosefu wa usalama, kwasababu hatujui historia yao.

Amesema kuwa mataifa ya Ulaya hayana uwezo wa kutosha kushughulikia wahamiaji, ambao wakati mwingine wanalazimika kuishi mitaani, huku baadhi wakitumbukia katika uhalifu. Miongoni mwa waandamanaji alikuwemo kiongozi wa chama hicho Andre Ventura.

Chama chake kiliongeza viti vyake kwa zaidi ya mara nne kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Forum

XS
SM
MD
LG