Katika maandamano hayo yaliyoandaliwa na Waislamu na makundi ya mrengo wa kushoto, walioshiriki waliimba: "Palestina inapinga" na "sote tunapinga kurasimishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia" huku wakichoma bendera ya IsraeIi.
"Nakemea undumilakuwili wa serikali nyingi za Magharibi kuhusu Wapalestina," Charki Lahrech alisema kwenye maandamano hayo, akisema baadhi ya mataifa yanafumbia macho mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Israeli baada ya mashambulizi ya wanamgambo wa Hamas.
"Huwezi kukemea vitendo vya Hamas na kutokemea mauaji ya Israeli ya raia wakiwemo watoto, wanawake na wazee... Huu ni ujumbe wa mshikamano na watu wa Palestina kuwaambia hawako peke yao."
Morocco, ambayo ina mkataba wa ushirikiano wa kiulinzi na Israeli, inaunga mkono suluhu ya mataifa mawili katika Mashariki ya Kati na imehimiza amani na ulinzi wa raia wote.
Forum