Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 28, 2024 Local time: 11:30

Maelfu ya wafuasi wa Imran Khan waandamana Pakistan


Wafuasi wa Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan aliyefungwa jela Imran Khan's wakiandamana Islamabad Jumapili . Nov. 24, 2024.
Wafuasi wa Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan aliyefungwa jela Imran Khan's wakiandamana Islamabad Jumapili . Nov. 24, 2024.

Maelfu ya wafuasi wa waziri mkuu wa zamani wa Pakistan aliyefungwa jela Imran Khan, Jumapili wameandamana kuelekea Islamabad wakiitishia kuachiliwa kwake pamoja na wafungwa wengine wa kisiasa.

Hali hiyo ilipelekea serikali kufunga shughuli kwenye mji huo pamoja na kukata kwa muda huduma za internet. Khan ameomba wafuasi wa chama chake cha Tehreek-e-Insaf au PTI, kukusanyika kwenye bustani ya umma ya D-Chowk, mjini Islamabad, na waendelee kubaki hapo hadi pale serikali itakapo sikia kilio chao.

Serikali ya muungano ya waziri mkuu Shehbaz Sharif ilituma maelfu ya polisi pamoja na vikosi vingine kuzuia ghasia na kufunga barabara kuelekea Islamabad kabla ya maandamano hayo ya upinzani. Polisi pia walipiga marufuku mikusanyiko ya kila aina mjini humo kabla ya maandamano hayo.

Serikali pia imefunga barabara kadhaa kubwa kwenye mji huo huku ikitumia makontena kuzuia waandamanaji kufika kwenye bustani hiyo iliopo karibu na majengo ya bunge na Mahakama ya Juu, miongoni mwa majengo mengine muhimu ya serikali.

Licha ya juhudi hizo za kiusalama, viongozi wa upinzani wa PTI pamoja na wafuasi wao wameapa kufika kwenye bustani hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG