Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 20, 2024 Local time: 11:20

Madai ya wanajeshi wa Korea kaskazini kusaidia Russia nchini Ukraine


Rais wa Russia Vladimir Putin (kushoto) na mwenzake wa Korea kaskazini Kim Jon Un
Rais wa Russia Vladimir Putin (kushoto) na mwenzake wa Korea kaskazini Kim Jon Un

Mawaziri wa mambo ya nje wa Ufaransa na Ukraine wamesema kwamba hatua ya Korea kaskazini kutuma wanajeshi kusaidia Russia katika uvamizi wake nchini Ukraine, itapelekea vita kuongezeka.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean Noel Barrot, ambaye ametembelea Ukraine kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kwa nafasi hiyo mwezi Septemba, anatarajiwa kutembelea mashariki mwa Ukraine hapo kesho, ambapo Ufaransa itafadhili vituo viwili vipya vya kuwalinda watoto walioathiriwa na vita.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, ameshutumu Korea kaskazini kutokana na hatua yake ya kutuma wanajeshi 10,000 kusaidia Moscow katika vita vyake nchini Ukraine, japo mkuu wa NATO Mark Rutte amesema kwamba hakuna ushahidi wa Pyongyang kutuma wanajeshi wake kufikia sasa.

Mapema wiki hii Zelenskyy aliwasilisha mpango wake wa ushindi ambao alisema utawezesha Ukraine kumaliza vita kabla ya mwaka ujao.

Forum

XS
SM
MD
LG