Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:13

Kamati ya Usalama: 'Madai ya Trump dhidi ya Obama hayana ushahidi'


Obama -Trump
Obama -Trump

Madai ya Rais Donald Trump wa Marekani kwamba mtangulizi wake, Rais mstaafu Barack Obama, alimrikodi wiki kadhaa kabla ya uchaguzi wa Novemba mwaka jana hayana ushahidi, uongozi wa juu wa kamati ya Usalama ya Bunge la Marekani umesema Jumatano.

“Hatuna ushahidi wowote unaonyesha udukuzi huo umefanyika,” Mbunge wa Republikan Devin Nunes, mwenyekiti wa jopo amesema. “ Si dhani kwamba Jengo la Trump Tower lilirikodiwa,” jumba refu ambalo ni makao makuu ya rais huko New York.

Mbunge Adam Schiff, mwanakamati wa ngazi ya juu, amekubaliana na kauli ya kuwa hakujawa na udukuzi katika jengo hilo. “Mpaka sasa, sijaona ushahidi (wa amri iliyotolewa na Obama kurikodi), hakuna msingi wowote katika hilo,” amesema.

Nunes na Schiff wamesema wanasubiri kupokea taarifa kutoka Idara ya Sheria nchini Jumatatu ijayo iwapo idara hiyo inajua chochote kuhusu amri ya mahakama iliyoruhusu Trump arikodiwe. Lakini wamesema hawajaweza kugundua udukuzi huo mpaka sasa wanavyo endelea na uchunguzi.

Uchunguzi huo unaofanywa na bunge umefuatia ombi la White House baada ya Trump kuibuka na madai ya kurikodiwa Machi 4 kwenye ujumbe wake wa Twitter.

Kamati ya Usalama ya Bunge pia inachunguza uhusiano kati ya wasaidizi wa kampeni ya Trump na maafisa wa Russia wakati bilionea maarufu mwenye biashara za majumba alipokuwa katika kinyang’anyiro cha kuingia White House na katika wiki kadhaa baadae alishinda uchaguzi kabla ya kuchukua madaraka ya urais January 20.

Nunes amesema kuwa James Comey, mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ,FBI, chombo cha juu kinacho simamia utekelezaji wa sheria, atatoa ushuhuda Jumatatu mbele ya kamati ya usalama juu ya madai ya kurikodiwa na uchunguzi unaohusu Russia kuingilia kati uchaguzi kwa nia ya kumfanya Trump ashinde.

Amesema kuwa jopo la wataalamu linategemea kufahamishwa Ijumaa na wachunguzi wa Marekani majina ya wasaidizi wa Trump waliokuwa na mawasiliano na maafisa wa Russia zaidi ya kile kinachojulikana juu ya mawasiliano na mazungumzo kati ya mshauri wa taifa wa Trump aliyeondolewa madarakani, mstaafu Jenerali Michael Flynn, na balozi wa Russia Washington.

Trump alimfukuza kazi Flynn baada ya kumdanganya Makamu wa Rais Mike Pence kuhusu mawasiliano yake na balozi, Sergey Kislyak

XS
SM
MD
LG