Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema kwamba Ufaransa na Algeria zinapaswa kuondokana na historia yao "chungu" na kutazama siku zijazo siku wakati akianza ziara ya siku tatu katika nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika.
Maumivu ya utawala wa kikoloni wa Ufaransa nchini Algeria na vita vikali vya uhuru vilivyomalizika mnamo mwaka wa 1962, yamekumba uhusiano kati ya nchi hizo mbili kwa miongo kadhaa, kwelekea katika mzozo wa kidiplomasia uliozuka mwaka jana.
"Tuna historia ngumu na chungu ya pamoja. Na wakati fulani imetuzuia kutazama siku zijazo," Macron alisema baada ya kukutana na mwenzake wa Algeria Rais Abdelmadjid Tebboune.
Akiwa amesimama kando ya Macron mbele ya kasri la Afrika Kaskazini lililo na utata, Tebboune alisema "Tunatumai ziara hii itafungua mitazamo mipya ya ushirikiano kati ya nchi yetu na Ufaransa".
Uhusiano na Algeria umekuwa muhimu zaidi kwa Ufaransa kwa sababu vita vya Ukraine vimeongeza mahitaji katika Ulaya, ya gesi kutoka Afrika Kaskazini, na kwa sababu ya kuongezeka kwa uhamiaji kupitia Bahari ya Mediterania.
Algeria wakati huo huoinatazamia kufaidika na bei ya juu ya nishati katika bara ulaya, kwa kuvutia waekezaji kununua bidhaa hiyo kuktoka kwake. Macron kwa muda mrefu alitaka kufungua ukurasa na Algeria, na mnamo 2017 alielezea vitendo vya Ufaransa wakati wa vita vya 1954-62, ambavyo vilisabisha vifo vya maelfu ya Waalgeria kama "uhalifu dhidi ya ubinadamu".