Milipuko miwili imeutikisa mji mkuu wa Uganda Kampala siku ya Jumanne, na kusababisha vifo vya watu 6 na karibu 30 kujeruhi wa katika kile polisi walichokitaja kuwa ni shambulizi la katika mji huo, ikiwa ni milipuko ya hivi karibuni zaidi katika mfululizo wa milipuko iliyolenga nchi hiyo.
Mkuu wa polisi wa Uganda anasema Milipuko hiyo ilitokea katika mtaa wa biashara kati kati ya Kampala karibu na kituo kikuu cha polisi na eneo la majengo ya bunge.
Tunachoweza kusema hili lilikuwa shambulio lakini nani anahusika ni suala ambalo linachunguzwa, Msaidizi wa Inspekta Mkuu wa polisi wa Uganda Edward Ochom aliambia AFP.
Msemaji wa wizara ya afya Ainebyoona Emmanuel alisema kwenye Twitter kwamba hospitali ya Mulago ya Kampala inahudumia watu 24, wanne wakiwa katika hali mbaya.
Kufuatia kitendo hicho cha kigaidi cha bahati mbaya na cha uoga, wahudumu wetu wa afya wanafanya kazi usiku kucha kuokoa maisha ya waliojeruhiwa, alisema.
Mlipuko uliotokea karibu na kituo cha polisi ulivunja vioo huku ile iliyo karibu na lango la bunge ilipelekea magari yaliyokuwa yameegeshwa karibu yakiteketea kwa moto, Ochom alisema.