Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 16:01

Mabadiliko ya hali ya hewa kusababisa hasara ya kifedha kwa mataifa


Jengo la benki kuu ya dunia mjini Washington DC
Jengo la benki kuu ya dunia mjini Washington DC

Benki ya dunia Jumatatu imesema kwamba uchafuzi wa hewa mashariki ya kati pamoja na kaskazini mwa Afrika unasababisha hasara ya dola bilioni 141 za kimarekani kila mwaka.

Kiasi hicho ni takriban asilimia 2 ya mapato ya ndani, wakati ikihimiza umuhimu wa kutochafua mazingira wakati eneo hilo linapojikwamua kutokana na athari za janga la Corona. Ripoti hiyo imeongeza kusema kwamba uchafuzi wa mazingira utagharimu baadhi ya mataifa kwenye eneo hilo kama vile Misri,Lebanon na Yemen zaidi ya asilimia 3 ya mapato ya ndani kila mwaka.

Uzalishaji wa nchi hushuka pale wakazi wanaposhindwa kufanya kazi kutokana na maradhi yaliyosababishwa na uchafuzi wa hewa, wakati gharama ya matibabu ikiwa mzigo mkubwa kwa watu binafsi au hata serikali,ripoti hiyo imeongeza.

Takwimu zinaonyesha kwamba mtu wa kawaida huenda akapoteza siku 60 za maisha yake wakati akiugua kutokana na uchafuzi wa hewa, wakati wakazi wa mijini wakisemekana kuvuta uchafu mara 10 juu ya viwango vinavyosemekana kuwa salama kutoka shirika la Afya duniani.

Imetayarishwa na Harrison Kamau

XS
SM
MD
LG