Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 02:24

Maandamano yameongezeka Msumbiji


Uharibifu kutokana na maandamano ya kisiasa Msumbiji
Uharibifu kutokana na maandamano ya kisiasa Msumbiji

Wanajeshi wanaendelea kushika doria kwenye barabara za Msumbiji kukabiliana na maandamano ya wiki kadhaa dhidi ya chama tawala ambacho kinashutumiwa kwa wizi wa kura.

Msemaji wa jeshi la Msumbiji Jenerali Omar Saranga amesema kwamba Jeshi linawasaidia polisi kukabiliana na waandamanaji.

Ikulu ya rais imewekwa chini ya ulinzi mkali huku maafisa wa usalama wakipiga doria barabarani. Watu wengi wameamua kujifungia majumbani mwao.

Maelfu ya waandamanaji wamechoma moto barabarani na kufunga barabara za mji mkuu wa Maputo.

Polisi wametumia gesi ya kutoa machozi kukabiliana na waandamanaji wanaopinga ushindi wa mgombea wa urais wa chama cha Frelimo Daniel Chapo.

Chama cha Frelimo kimetawala Msumbiji tangu nchi hiyo ilipopata uhuru kutoka kwa Ureno mwaka 1975.

Forum

XS
SM
MD
LG