Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 21, 2024 Local time: 20:42

Maandamano ya wanafunzi Marekani dhidi ya Israel na Hamas yanaendelea


Maandamano yanaendelea katika kampasi ya chuo kikuu cha Columbia nchini Marekani.
Maandamano yanaendelea katika kampasi ya chuo kikuu cha Columbia nchini Marekani.

Picha za video ziliwaonyesha waandamanaji katika chuo cha Manhattan cha Columbia walifunga  mikono mbele ya ukumbi wa Hamilton.

Darzeni ya waandamanaji walivamia jengo katika Chuo Kikuu cha Columbia mjini New York mapema leo Jumanne, wakiziba milango ya kuingia ndani na kupeperusha bendera ya Palestina nje ya dirisha katika maandamano ya hivi karibuni dhidi ya vita vya Israel na Hamas ambayo yamesambaa hadi vyuo vikuu kote nchini Marekani.

Picha za video ziliwaonyesha waandamanaji katika chuo cha Manhattan cha Columbia walifunga mikono mbele ya ukumbi wa Hamilton mapema Jumanne na kubeba samani na vizuizi vya chuma kwenye jengo hilo moja ya samani ambayo ilikaliwa wakati wa maandamano ya haki za kiraia ya mwaka 1968 na kupinga vita vya Vietnam kwenye chuo hicho.

Machapisho kwenye ukurasa wa Instagram kwa waandaaji wa maandamano muda mfupi baada ya usiku wa manane yaliwahimiza watu kuilinda kambi hiyo na kujiunga nao katika ukumbi wa Hamilton.

Forum

XS
SM
MD
LG