Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:32

Maandamano dhidi ya kukamatwa Bobi Wine yaendelea Uganda


Bobi Wine akiwa katika maandamano Uganda
Bobi Wine akiwa katika maandamano Uganda

Biashara zilisimama Jumamosi mjini Mukono, Uganda wakati maandamano yalipoanza kupinga kuendelea kuwekwa kizuizini Robert Kyagulanyi (Bobi Wine).

Bobi Wine ni mwanasiasa wa kambi ya upinzani nchini Uganda.

Maandamano hayo yalisababisha watu wenye silaha kupiga risasi za moto na kutupa mabomu ya machozi ili kuwasambaza waandamanaji hao.

Operesheni hiyo iliongozwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mukono Rogers Sseguya na maafisa wengine waliokuwa zamu wa vituo mbalimbali vya polisi wilayani Mukono.

Moses Kiwanuka ambaye ni mmoja wa wakazi wa eneo hilo amesema hawawezi kukaa na kutizama wakati serikali ikiwaweka kizuizini na kuwatesa watu.

Wakazi hao walianza kwa kufunga barabara ya Mukono-Kayunga na kisha wakaendelea kuzuia njia kuu ya Kampala-Jinja.

Mkuu wa polisi wa wilaya hiyo Sseguya aliagiza wenye maduka ambao waliacha waliendelea kufanya biashara kufunga maduka yao na kuwaambia kuwa biashara zao zitaangamizwa.

Ijumaa, polisi hao waliwakamata waandamanaji kadhaa pembezoni mwa mji huko Kamwokya.

Wakazi hao walikamatawa katika msako uliosimamiwa na mkuu wa polisi wa mkoa wa Kampala ya Kaskazini Michael Musana.

Maandamano hayo yalianza Alhamisi baada ya habari kuenea kwa kukamatwa kinyama, kuteswa na kuwekwa kizuizini Kyagulanyi na jeshi la nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG