Maambukizi yalikumba taifa hilo lenye idadi kubwa zaidi ya watu ulimwenguni toka chama tawala cha kikomunisti kilipo ondoa kwa ghafla sera ya maambukizi sifuri ya Covid mwezi uliopita.
Hospitali zilijaa wagonjwa, na sehemu za kuchomea maiti zilifurika katika miji mikubwa ikijumuisha Beijing, licha ya kwamba kiwango cha mlipuko imekuwa vigumu kuthibitishwa kutokana na taarifa rasmi kuaminika kuwa ndogo ikilinganishwa na hali halisi.
Lakini kumekuwa na ishara za maambukizi kupungua, huku serekali wiki iliyopiya ikisema kwamba idadi ya vifo vya Covid-19 nchini kote imeshuka kwa karibu asilimia 80 toka Januari.