Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:16

Maalim Seif asema hajakata tamaa, ana matumaini ya ushindi


 Seif Sharif Hamad
Seif Sharif Hamad

Maalim Seif Sharif Hamad, ni mmoja wa wanasiasa wakongwe na mashuhuri wa Zanzibar na Tanzania akiwa amegombania mara tano kiti cha rais na kushindwa, lakini anadai aliibiwa ushindi. 

Kiongozi huyo wa upinzani anaingia katika historia kwa kuwa miongoni mwa wagombea wa upinzani wa nchi nyingi za Afrika walioibiwa ushindi mara kadhaa, lakini wana matumaini siku moja watapata ushindi kama alioupata aliyekua rais wa Senegal, Abdoulaye Wade aliyegombania mara nne hadi kushinda mwaka 2000.

Abdoulaye Wade
Abdoulaye Wade

Maalim Seif ni miongoni mwa Wazanzibari waliozuiliwa kuendelea na masomo ya juu kwa karibu miaka 9 kwa kukataa kufanya kazi ya umma kutokana na kuondoka kwa maafisa wa utawala wa kikoloni wa Uingereza 1964.

Hatimaye alihitimu na kupata shahada ya kwanza ya sayansi ya siasa kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Muda mfupi baada ya kuhitimu masomo ya juu aliingia katika siasa akiwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na kuteuliwa waziri wa elimu, akiwa pia mbunge katika bunge la taifa la Tanzania.

Mshauri Wake wa karibu na mjumbe wa kamati kuu ya chama cha ACT-Wazalendo, Ismael Jussa anasema Maalim Seif ameendelea kuwa na nguvu katika siasa kwa miaka 43 sasa ni kutokana na “kuungwa mkono na wanananchi waliowengi wa Zanzibar, na hiyo inathibitika kwamba ni mwanasiasa wa pekee ambaye kila umri ukiongezeka ndipo nyota yake inazidi kun’gara.”

Jussa anasema kila mara akigombania uchaguzi kura zake zinaongezeka na alifikia kilele katika uchaguzi wa 2015, pale watawala walilazimika kuufuta uchaguzi wakati Maalim Seif alipoweza kumshinda mgombea kiti wa chama cha CCM kwa zaidi ya kura elfu 25.

Kama katika uchaguzi wa miaka kabla ya hiyo Maalim Seif na chama chake cha CUF walicho kianzisha mwaka 1992 walipinga matokeo na wafuatiliaji wa kimataifa pia kusema kulikuwa na wizi wa kura. Uchaguzi mpya uliitishwa na akakata kushiriki na ushindi ukawa wa Dkt Ali Mohamed Shein.

Lakini kabla ya hapo wakati wa uchaguzi wa 2000 ulodaiwa kuwa pia na wizi wa kura, ghasia zilizuka wakati wa maandamano ya Januanri 2001 ambapo wafuasi 45 wa CUF waliuliwa na maafisa wa usalama na wengine wengi kukimbia uhamishoni.

Baada ya ghasia hizo makubaliano yalifikiwa kati ya Serikali ya CCM na CUF chini ya makubaliano ya MUAFAKA wa pili yaliyotaka mageuzi ya katiba na kushirikiana madaraka. Lakini CUF inadai serikali haikutekeleza kikamilifu makubaliano hayo na baada ya kuwepo kwenye serikali Maalim Seif hadi uchaguzi wa 2015.

Jussa anasema imani ya wananchi na uwaminifu wanaompa ndio imemsababisha kugombania tena kiti cha rais, akisisitiza kwamba kutokana na unyenyekevu wa kiongozi huyo na kuishi maisha ya kawaida sawa na Wazanzibari wa tabaka la chini ndio imempatia nguvu kwenye siasa.

Wakosoaji wake wanasema Maalim Seif anauchu wa madaraka na ndio maana anaendelea kugombania nafasi hiyo na hajamtayarisha mtu kuchukua nafasi yake. Hilo ni jambo ambalo Jussa anapinga akimtetea kuwa ni mwanasiasa moja wapo wa Tanzania aliyewawezesha wanasiasa vijana na kuwatayarisha kuchukua uongozi.

Seif Sharif Hamad, kushoto, alipokutana na Rais Magufuli Ikulu Dar es Salaam Tanzania.
Seif Sharif Hamad, kushoto, alipokutana na Rais Magufuli Ikulu Dar es Salaam Tanzania.

Anasema kasoro yake kubwa ni kwamba yeye ni mtu anaependa maridhiano na maelewano ndio maana kashindwa mara hizo tano lakini safari hii amenuia kwamba hatokubali kushindwa ikiwa wananchi watamuunga mkono na atawaachia wao uamuzi.


XS
SM
MD
LG