Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 01:07

Maafisa wa zamani White House wanaitwa kuhojiwa na kamati ya sheria bungeni


Hope Hicks, mkurugenzi wa zamani wa mawasiliano White House
Hope Hicks, mkurugenzi wa zamani wa mawasiliano White House

Mwenyekiti wa kamati ya sheria bungeni m-Democrat Jerrold Nadler alisema kamati inataka kusikia kutoka kwa maafisa wa juu wawili ambao ni mkurugenzi wa mawasiliano wa zamani wa White House, Hope Hicks na mkuu wa utawala wa zamani wa Donald McGahn, Annie Donaldson

Kamati ya sheria ya baraza la wawakilishi la bunge la Marekani imetoa hati ya kisheria ikiwataka maafisa wawili wa zamani wa White House kufika mbele ya kamati hiyo baada ya wakili wa zamani wa White House, Donald McGahn kupuuzia hati kama hiyo siku ya Jumanne iliyomtaka kutoa ushahidi kuhusu shutuma zinazomkabili Rais Donald Trump kwamba alizuia sheria kuchukua mkondo wake.

Mwenyekiti wa kamati hiyo m-Democrat Jerrold Nadler alisema kamati hiyo inataka kusikia kutoka kwa mkurugenzi wa mawasiliano wa zamani wa White House, Hope Hicks na mkuu wa utawala wa zamani wa Donald McGahn, Annie Donaldson.

Sauti ya Amerika-VOA ilizungumza na Profesa David Monda akiwa New York nchini Marekani na kumuuliza kwanza iwapo maafisa hao wawili wataitikia wito wa kamati ya sheria bungeni au watafuata nyayo za mtangulizi wao, McGahn

please wait

No media source currently available

0:00 0:04:32 0:00

Wawili hao wametakiwa kutoa hati na kuhojiwa na wabunge kabla ya mwezi ujao.

Hicks kabla ya kujiuzulu White House Machi 2018 aliiambia kamati ya ujasusi ya baraza la wawakilishi kwamba wakati mwingine alitunga uongo ili kumlinda Trump.

Nae Donaldson anaaminika ana kurasa nyingi za taarifa zinazohusiana na Trump na jinsi alivyokuwa akijibu uchunguzi wa Muller.

Jerrold Nadler, mwenyekiti wa kamati ya sheria bungeni
Jerrold Nadler, mwenyekiti wa kamati ya sheria bungeni

Wakati huo huo Nadler anatishia kumfungulia mashtaka McGahn kwa kukataa kwake kutoa ushahidi bungeni Jumanne baada ya Trump kumueleza apuuzie hati maalumu ya kisheria inayomtaka afike bungeni kutoa ushahidi na wizara ya sheria Marekani ilisema McGahn hawezi kulazimishwa kufika bungeni.

Timu ya Mueller ilimuhoji McGahn kwa saa 30 kuhusu muingiliano wake na Trump.

Mbunge mwingine m-democrat katika kamati ya sheria ya baraza la wawakilishi, David Cicilline alikiambia kituo cha televisheni cha MSNBC cha Marekani kwamba kama McGahn alimsikiliza Rais Trump na kukaidi hati ya kisheria inayomtaka atoe ushahidi basi hatua ya kufunguliwa mashtaka Rais Donald Trump inatakiwa kuanza.

XS
SM
MD
LG