Maafisa katika jimbo la Baluchistan nchini Pakistan wanalaumu mauaji ya alfajiri ya leo kwa vinyozi wasiopungua saba kutoka jimbo la Punjab yakiwahusisha washukiwa waasi wa Baluch.
Tukio hilo limetokea katika mji wa pwani wa Gwadar, ambapo kampuni moja ya China imejenga na kuendesha bandari ya kina kirefu cha maji katika bahari ya Arabia. Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo la leo Alhamisi.
Makundi ya waasi ya Baluch yaliyopigwa marufuku, ikiwemo Baluch Liberation Army- Jeshi la Ukombozi la Baluch, au BLA yamedai kuhusika na kuwalenga Punjabi na walowezi kutoka sehemu nyingine za Pakistan huko Baluchistan katika siku za nyuma, wakidai walikuwa na uhusiano na vikosi vya usalama vya Pakistan.
Polisi wa Gwadar waliwaambia waandishi wa habari kuwa waathirika, ambao pia ni pamoja na mmoja aliyejeruhiwa, walikuwa wamelala wakati washambuliaji walipovamia makazi yao na kuwarushia risasi kabla ya kutoroka.
Forum