Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 06:45

M23 yaishutumu serikali ya DRC kugomea mazungumzo


Waasi wa kundi la M23 katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC
Waasi wa kundi la M23 katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC
Waasi wa kundi la M23 la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC wanaishutumu serikali ya Congo kwa kukataa mashauriano kwenye mazungumzo ya amani ya mjini Kampala nchini Uganda.

Mazungumzo ya mjini Kampala yalikwama mwezi April mwaka huu na yalipangwa kuanza tena Kampala wiki hii. Kundi la M23 linasema timu ya serikali ya Congo iliwasili Kampala Jumatano ili tu kumweleza mpatanishi wa mazungumzo Uganda kwamba hawataweza tena kufanya mashauriano na kundi la M23.

Katika barua iliyotumwa Alhamis kwa mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la maziwa makuu waasi pia wanasema jeshi la serikali na washirika wake wanajiandaa kikamilifu kufanya mashambulizi wakati wowote.

Barua hiyo inaishutumu zaidi serikali kwa kuwakamata zaidi ya watu 50 mjini Goma wengi wao wazungumzaji wa lugha ya Kinyarwanda ambapo baadhi yao wanasema wamehamishiwa Kinshasa huku wengine wamechukuliwa kwenda maeneo yasiyojulikana.

Wapiganaji wengi wa M23 wanatoka Rwanda. Ripoti kadhaa za wataalamu wa Umoja wa Mataifa zinaishutumu Rwanda kwa kuwasaidia waasi wa kundi la M23 madai ambayo serikali ya Rwanda inayakanusha.

Akizungumza na Sauti ya Amerika-VOA - msemaji wa serikali ya Congo Lambert Mende alisema serikali imemweleza mpatanishi wa mazungumzo hayo kwamba hakuna swali la kuanza tena kwa mazungumzo ambayo tayari yalishamalizika wakati waasi wa kundi la M23 walipoondoka kwenye meza ya mashauriano.

Hata hivyo Menda alikanusha shutuma kwamba majeshi ya serikali na washirika wake yanajiandaa kwa mashambulizi.
XS
SM
MD
LG