Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:49

Lissu mtetezi wa wananchi walioathirika na uwekezaji katika migodi


Tundu Lissu
Tundu Lissu

Tundu Lissu mmoja kati ya wakosoaji wakuu wa rais John Pombe Magufuli, anafahamika zaidi hivi sasa kama mtu aliyenusurika shambulio baya la bunduki hapo Septemba 7, 2017. 

Alishambuliwa na watu wasiojulikana ambao hadi hivi sasa hawajapatikana, na kujeruhiwa vibaya hadi kulazimika kusafirishwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi.

Lissu alirudi nyumbani tarehe 7 April 2020, akitokea Brussels, Ubelgiji ambako kwa miaka 3 amekua akipatiwa matibabu kutokana na majeraha yake, na alipowasili Dar es Salaam alipokelewa kama shujaa na mamia ya wafuasi wake.

Umaarufu wa mbunge huyo wa zamani wa jimbo la Singida Mashariki hata hivyo haukuanza baada ya shambulio hilo, bali ulianza kutokana na harakati zake za kuwatetea wananchi waliokua wameathirika na uwekezaji katika migodi ya madini. Pia alikuwa wakili wa mstari wa mbele kutetea haki za ardhi na mazingira kabla ya kujitosa kwenye siasa.

Moja kati ya hoja zake kuu bungeni ni hapo tarehe 14 Juni mwaka 2017, alipowasilisha haki za wachimbaji madini, ambapo alikemea sana utendaji kazi wa kamati iliyoteuliwa na rais Magufuli kuchunguza matatizo kwenye sekta ya madini.

Alichaguliwa mbunge kwa mara ya kwanza mwaka 2010 akiwa mwanachama wa upinzani wa chama cha CHADEMA, na mara moja akawa ni sauti kuu ya upinzani hadi kua mnadhimu wa kambi ya upinzani bungeni. Akiwa nje ya nchi akipatiwa matibabu Lissu alivuliwa ubunge tarehe 28 Juni, 2019, kwa madai ya kutohudhuria vikao vya bunge pamoja na kutojaza fomu za maadili juu ya mali na madeni kama inavyotakiwa kikatiba. Juhudi zake za kuzuia kuvuliwa ubunge ziligonga mwamba mahakamani.

Akiwa anapata matibabu mwanasheria aliyegeuka kua mwanasiasa, aliendelea kuikosoa serekali ya Tanzania na kufanya mahojiano na vyombo mbali mbali vya kimataifa akitembelea nchi za Ulaya na Marekani na kukutana na watanzania wanaoishi nje.

Katika mahojiano na kusisimua kati ya balozi wa Tanzania hapa Marekani Wilson Masilingi pale Lissu alipotembelea Sauti ya Ameika Februari 2019 alikemea serikali kwa kutofanya uchunguzi kuhusu jaribio la kutaka kumuua akiwa mbunge.

Huku Mashlingi akidai kwamba mbunge huyo wa upinzani anafanya ziara ya mataifa ya magharibi kwa lengo la kuichafua serekali.

Tangu akiwa nje ya nchi mbunge huyo wa zamani wa Singida, alitangaza nia yake ya kugombania kiti cha rais na aliporudi nyumbani chama chake cha CHADEMA kilimteua akikiwakilishe chama.

Na mara tu baada ya tume ya taifa ya uchaguzi(NEC) kuidhinisha maombi yake ya kugombania urais Tundu Lissu alianza kampeni kote nchini akieleza matumaini ya kumshinda rais Magufuli.

Anagombania nafasi hiyo ya juu ya kuiongoza nchi akiwa vado anakabiliwa na mashtaka sita anayodai ni yenye malengo ya kisisasa.

Patrick Nduwimana, VOA, Washington DC.

XS
SM
MD
LG