Jeshi la Israel lilishambulia zaidi ya ngome 1,300, huku shirika la habari la serikali ya Lebanon likiripoti mapigano makali katika majimbo mengi eneo la kusini mwa nchi.
Miongoni mwa waliouawa ni watoto 35 na wanawake 58, maafisa wa wizara ya afya ya Lebanon walisema.
Jeshi la Israel limeonya wakazi wa bonde la Bekaa mashariki mwa Lebanon kukaa mbali na ghala za silala za Hezbollah.
“Tunaendelea kufuatilia maandalizi ya Hezbollah uwanjani ili kuzuia mapema mashambulizi yao kwenye eneo la Israel, na tumezidisha sana mashambulizi yetu dhidi ya Hezbollah,” msemaji wa jeshi la Israel Amirali Daniel Hagari aliwambia waandishi wa habari.
Katika ujumbe uliorekodiwa kwa raia wa Lebanon, waziri mkuu wa Israel Banjamin Netanyahu amewataka kuzingatia wito wa Israel wa kuondoka, akisema lazima “wachukulie onyo hilo kuwa sio mzaha.”
Forum