Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 03:26

Lamont Marcell Jacobs anyakua taji la Usain Bolt kwenye mbio za Olimpiki za mita 100

APTOPIX Tokyo Olympics Athletics
APTOPIX Tokyo Olympics Athletics

Jacobs anakua Mtaliana wa kwanza kabisa kunyakua taji hilo ambalo limekua likishiikiliwa kwa zaidi ya muongo mmoja na bingwa wa dunia Usain Bolt wa Jamaica.

Kwa mshangao mkubwa, Lamont Marcell Jacobs anyakua medali ya dhahabu katika mbiyo za mita 100 akitumia muda wa sekunde 9.80 zilizokua zikisubiriwa kwa hamu kubwa kwenye michezo ya Olimpiki mjini Tokyo.

Katika fainali hiyo ya kwanza baada ya enzi ya Bolt, Mmarekani Fred Kerley alichukua nafasi ya pili akitumia sek 9.84, na medali ya shaba kuchukuliwa na Andre Grasse kutoka Canada aliyechukua medali hiyo hiyo mwaka 2016.

Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2000 hapa kuwepo na mkimbiaji kutoka Jamaica katika finali ya mbio za mita 100 baada ya bingwa wa dunia Yohan Blake kushindwa katika awamu ya nusu finali, hasa baada ya medali zote tatu katika mbiyo za wanawake mita 100 kuchukuliwa na wakimbiaji wa Jamaica siku moja kabla.

Tukio la kusisimua zaidi ni kwamba wanariadha kutoka mabara ya Afrika, Ulaya, Asia na Amerika ya kaskazini walishiriki kwenye finali hiyo mashuhuri.

Akani Simbine wa Afrika Kusini altoka nafasi ya nne akifuatwa na Su Bingtian wa China.

Na katika mchuano mwengine wa kuvutia Jumapili ulikua ni kuruka juu, pale wanariadha watatu waliweza kuruka umbali sawa wa mita 2.37 lakini dhahabu kutolewa kwa Mutaz Essa Barshim wa Qatar na Gianmarco Tamberi wa Italy.

Kwa upande wa medali jumla Marekani inaongoza ikiwa na medali 59 ikifuatiwa na Uchina yenye medali 51, lakini Uchina inaongoza kwa kunyakua medali zaidi za dhahabu. Uchina inamedali 24 za dhahabu wakati Marekani ina 20.

Afrika ya kusini ndio inaongoza nchi za kiafrika hadi sasa ikiwa na jumla ya medali 3 moja ya dhahabu na mbili za fedha.

Kwa mshangao mkubwa, Mtaliana Lamont Marcell Jacobs anyakua medali ya dhahabu katika mbiyo za mita 100 akitumia muda wa sekunde 9.80 zilizokua zikisubiriwa kwa hamu kubwa kwenye michezo ya Olimpiki mjini Tokyo. Anakua Mtaliana wa kwanza kabisa kunyakua taji hilo ambalo limekua likizikiliwa kwa zaidi ya muongo mmoja na bingwa wa dunia Usain Bolt wa Jamaica.

Katika fainali hiyo ya kwanza baada ya enzi ya Bolt, Mmarekani Fred Kerley alichukua nafasi ya pili akitumia sek 9.84, na medali ya shaba kuchukuliwa na Andre Grasse kutoka Canada aliyechukua medali hiyo hiyo mwaka 2016.

Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2000 hapa kuwepo na mkimbiaji kutoka Jamaica katika finali ya mbio za mita 100 baada ya bingwa wa dunia Yohan Blake kushindwa katika awamu ya nusu finali, hasa baada ya medali zote tatu katika mbiyo za wanawake mita 100 kuchukuliwa na wakimbiaji wa Jamaica siku moja kabla.

Cha kusisimua zaidi ni kwamba wanariadha kutoka mabara ya Afrika, Ulaya, Asia na Amerika ya kaskazini walishiriki kwenye finali hiyo mashuhuri.

Akani Simbine wa Afrika Kusini altoka nafasi ya nne akifuatwa na Su Bingtian wa China.

Na katika mchuano mwengine wa kuvutia Jumapili ulokua ni kuruka juu pale wanariadha watatu waliweza kuruka umbali sawa wa mita 2.37 lakini dhahabu kutolewa kwa Mutaz Essa Barshim wa Qatar na Gianmarco Tamberi wa Italy.

XS
SM
MD
LG