Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 18:56

Kuzuka tena kwa M23 ni kwa ajili ya Rwanda kulinda maslahi yake ripoti yaeleza


Nia ya Rwanda ya kulinda maslahi yake dhidi ya Uganda ndiyo chanzo kikuu cha waasi wa M23 kuzuka tena hivi karibuni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, makundi mawili ya utafiti yanayohusiana na Chuo Kikuu cha New York yamesema katika ripoti ya Jumanne.

Kundi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda, ambalo lilikuwa kimya kwa takriban muongo mmoja, lilianzisha mashambulizi katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwishoni mwa 2021 na toka kipindi hicho limeteka maeneo mbalimbali.

Uasi huo umeaonekana zaidi kama njia ya Rwanda kuonyesha ushawishi wake dhidi ya jirani yake wa kaskazini Uganda, taasisi ya Ebuteli yenye makao yake DRC na Kikundi cha Utafiti cha Congo chenye makao yake NYU yamesema.

Kigali, ambayo ilikubali kusitisha mapigano na Kinshasa inaamini kuwa kuwepo mashariki mwa DRC kwa Kikosi cha Kidemokrasia cha Ukombozi wa Rwanda (FDLR) ni tishio linaloendelea kwa mipaka ya Rwanda.

Forum

XS
SM
MD
LG