Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 19:58

Wasiwasi juu ya kuyumba uchunguzi dhidi ya Russia


Devin Nunes
Devin Nunes

Utaratibu usio wa kawaida wa kutangaza kwa umma shughuli ambazo kawaida ni siri za jumuiya ya usalama ya Marekani inaendelea kutia wasiwasi juu ya uwezo wa wabunge kuchunguza kuvuruga kwa Russia uchaguzi wa mwaka 2016.

Uchunguzi ambao tayari umefunikwa na madai ya Twitter ya Rais Donald Trump kuwa alikuwa amerikodiwa na mtangulizi wake, umeingia katika mkanganyiko zaidi Jumatano.

Mataifa ya nje

Wakati huo huo wabunge wanao ongoza uchunguzi wamedai kuwa “matukio yakurikodi” simu za Rais na wafanyakazi wanazopigiwa na watu wa mataifa ya kigeni” (Incidental Collection) ni sehemu ya shughuli za vyombo vya usalama.

“Kile nilicho kisoma kinanisumbua, na nafikiri ni kitu kitamsumbua rais na timu yake,” Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama, Devin Nunes, amewaambia waandishi baada ya kuchukua hatua isiyo ya kawaida kumpa rais muhtsari huo.

“Rais yeye mwenyewe na wengine katika timu ya mpito ya Trump walikuwa wamewekwa katika ripoti ya usalama,” Nunes amesema nje ya White House. “Baadhi ya ripoti hiyo inaonyesha kuwa haikuwa sawa.

Nunes amekataa kusema hasa wapi alipoipata hiyo taarifa ya kintelijensia, mara ikapelekea kupingwa na Mdemokrati wa ngazi ya juu wa Kamati ya Usalama ya Bunge, na kuita kitendo cha Nunes “chenye kutia wasiwasi mkubwa.”

Mchakato umekwenda ovyo

“Iwapo Mwenyekiti Nunes ataendelea kuwa upande wa White House badala ya kuwa na Kamati yake, hakuna njia tunaweza kufanya uchunguzi huu,” amesema Adam Schiff, Mdemocrat wa ngazi ya juu katika Kamati ya Usalama ya Bunge. “Tunahitaji kuwa na tume huru,” amesema.

Lakini Mbunge wa Republikan pia ameeleza wasiwasi wake kwamba mchakato umekwenda ovyo.

“Bunge haliaminiki tena kushughulikia hili peke yake, na sisemi hili juu juu, Seneta John McCain ameiambia MSNBC Jumatano jioni, akitaka iwepo tume huru au kamati maalumu kuchunguza hili.

Taarifa alizotoa Nunes zimekuja siku mbili baada ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai James Comey alipothibitisha kuwa maafisa wake wanachunguza kampeni ya Trump inayohusishwa na uwezekano wa kuwa na mafungamano na Russia. But Comey alikanusha madai ya ujumbe wa Twitter wa Trump kuwa alikuwa amerikodiwa.

Sina taarifa yoyote inayothibitisha tweets hizo. Na tumeangalia hilo kwa makini ndani ya FBI.

Trump anahisi yuko sahihi

Alipoulizwa kuhusu maoni ya Nunes, Trump amesema Jumatano alikuwa anahisi yuko sahihi.

“Lazima niwaambie kuwa kwa namna fulani ndio hivyo,” rais amesema. “Nimeridhika sana kwa ukweli wa kuwa walikuta kile walichokikuta.”

Nunes amesema alikuwa ameona dazeni fulani za ripoti za kiintelijensia ambazo zinadaiwa zilimtaja rais na watu wa timu yake. Lakini alisisitiza kuwa ripoti hizo “ hazikuwa na chochote kuhusu Russia na wala hazikuwa zinahusiana na uchunguzi wa Russia.”

“Nafikiri ni kitu muhimu sana, na lazima tuangalie hili litatuongoza wapi,” Mbunge wa Republikan Peter King amesema. “Inaonyesha kuwa kuna kitu hapo, na ni suali nani aliyeagiza hilo lifanyike

XS
SM
MD
LG