Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 08, 2025 Local time: 18:29

Kuwawezesha wanawake wa mashambani kukomesha njaa na umaskini


Maandamano na sherehe mbali mbali zimefanyika katika nchi mbali mbali kuhamasisha haki za wanawake katika siasa, uchumi na manedeleo.

Ujumbe wa mwaka huu uliotolewa na Umoja Mataifa unazungumzia kuwawezesha wanawake wa vijijini, kutokomeza njaa na umaskini, lengo ni kuwawezesha kielimu, kiuchumi na kimaendeleo.

Wanawake wa vijijini huko barani Afrika wanaelezewa kuwa wana mchango mkubwa katika mabadiliko ya uchumi, kijamii na mazingira, lakini kwa viwango tofauti kulingana na hali ilivyo katika maeneo ambayo wanaishi.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa mmoja wa mchango mkubwa wa umoja huo ni kuhakikisha usalama wa chakula, kutokomeza umaskini vijijini na kuboresha hali ya familia zao.

Umoja wa Mataifa unasisitiza kuwa wanawake hawa ambao ni wakulima, wazalishaji, watoa huduma, wawekezaji na pia baadhi yao wako katika sekta za ununuzi wanahitaji msaada wa kila mtu ili kuinua maisha yao.

Wakati yote haya yakitokea bado wanakabiliwa na changamoto nzito kutokana na jinsia yao na mtizamo wa jamii na ubaguzi wanaokumbana nao, ambapo matokeo yake ni kunyimwa fursa mbali mbali ambazo zinazoweza kuwasukuma mbele kimaendeleo.

Je juhudi gani zinafanyika kumuelimisha mwanamke juu ya haki zake na kuifahamu vyema elimu ya uraia ili aweze kushiriki katika shughuli mbali mbali.

Wakati ikielezewa kuwa uhamasishaji na elimu viko mstari wa mbele kumsaidia mwanamke kujikwamua, lakini mikakati gani itumike kuhakikisha kuwa wanawake hasa wale wa vijijini ambao ni walengwa wakuu mwaka huu, wanahusishwa katika masuala yanayowahusu na ya jamii kwa jumla.

Umoja wa Mataifa unaendelea kuzikumbusha serikali, makundi ya kijamii na watu mbali mbali kuwashirikisha kikamilifu wanawake wa vijijini katika nyanja ya kufanya maamuzi, ni muhimu sana endapo serikali zinataka kufanikisha lengo la maendeleo ya millennia.

Ili kupata mafanikio na maendeleo kwa upande wa wanawake suluhisho la kudumu ni kuwashikirikisha kikamilifu na kuwawezesha wanawake iwe wa mijini au vijijini kwa manufaa ya wote.

XS
SM
MD
LG