Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 15:42

Idadi ya wasomali wanaoliunga mkono al-Shaabab yaongezeka


Waandamanaji wanaowaunga mkono al-Shabaab wakihudhuria maandamano kupinga kuchomwa kwa koran kusini mwa Mogadishu nchini Somalia.
Waandamanaji wanaowaunga mkono al-Shabaab wakihudhuria maandamano kupinga kuchomwa kwa koran kusini mwa Mogadishu nchini Somalia.

Idadi ya wanamgambo wa Somalia wanaoliunga mkono kundi la Islamic State imeongezeka maradufu na wanapokea msaada wa kifedha na kijeshi kutoka Yemen, afisa wa kijasusi wa ngazi za juu ameiambia Sauti ya Amerika.

Abdi Hassan Hussein, aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Kijasusi ya Puntland inayoungwa mkono na Marekani, amesema wakati kundi hilo linalounga mkono Islamic State lilipoundwa mwezi Oktoba mwaka jana, lilikuwa na kati ya wanaume 20 na 30, lakini hadi hivi sasa limeshafungua kambi za mafunzo na kuandikisha wapiganaji zaidi. Alisema wapiganaji wa kundi hilo sasa wamefika kati ya 100 na 150. Hussein alisema vikundi vya kwanza tayari vimehitimu na kupewa vifaa vya kijeshi.

Hussein aliongoza idara hiyo ya PIA hadi mwaka jana wakati nafasi yake ilichukuliwa na mtu mwingine. Kazi yake muhimu ilikuwa ni kutambua vitisho vya wanamgambo na kupanga jinsi ya kukabiliana na visa vya kigaidi.

XS
SM
MD
LG