Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 02, 2024 Local time: 01:36

Kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani, Niger kumekamilika


Uondoaji wanajeshi wa Marekani kutoka Niger, umekamilika, afisa wa Marekani, amesema Jumatatu. Idadi ndogo ya wanajeshi waliopewa jukumu la kulinda Ubalozi wa Marekani wamebaki, msemaji wa Pentagon, Sabrina Singh, amewaambia waandishi wa habari.

Mapema mwaka huu, utawala wa kijeshi wa Niger ulihitimisha makubaliano yaliyoruhusu wanajeshi wa Marekani kufanya kazi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Miezi michache baadaye, maafisa kutoka nchi zote mbili wamesema katika taarifa ya pamoja kwamba wanajeshi wa Marekani wataondoka katikati ya Septemba.

Marekani ilikabidhi kambi zake za mwisho za kijeshi nchini Niger kwa serikali za mitaa mwezi uliopita, lakini takriban wanajeshi 22 wa Kimarekani walibakia Niger, hasa kwa ajili ya majukumu ya kiutawala yanayohusiana na uondokaji huo, Singh amesema.

Forum

XS
SM
MD
LG