Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 22:16

Kundi la waasi la Oromo Liberation Army lashutumiwa kwa kuua raia

Watu wakisherehekea kurejea kwa kundi lililokuwa limepigwa marufuku na serikali la Oromo Liberation Front (OLF) huko Addis Ababa, Ethiopia.Tarehe 15 Septemba, 2018. Picha na Yonas TADESSE / AFP.
Watu wakisherehekea kurejea kwa kundi lililokuwa limepigwa marufuku na serikali la Oromo Liberation Front (OLF) huko Addis Ababa, Ethiopia.Tarehe 15 Septemba, 2018. Picha na Yonas TADESSE / AFP.

Serikali ya mkoa mkubwa sana nchini  Ethiopia, Oromiya, siku ya Jumamosi ililishutumu kundi la waasi la Oromo Liberation Army (OLA) kwa kuua raia wengi katika mashambulizi yaliyofuatia kushindwa kwa mazungumzo ya amani nchini Tanzania.

Takriban watu 36 waliuwawa wakati washambuliaji wasiojulikana waliposhambulia vijiji vitatu katika wilaya ya Shirka huko Oromiya Novemba 24 na 27, wakaazi waliiambia Reuters.

Hailu Adugna, msemaji wa mkoa wa Oromiya, alilaumu mashambulizi kwa OLA, kundi lililopigwa marufuku la chama cha zamani cha upinzani ambacho kilirejea kutoka uhamishoni mwaka 2018.

Hakuna maoni ya mara moja kutoka kundi la OLA. Msemaji wa serikali ya shirikisho Legesse Tulu hakujibu ombi la kutoa maoni yake.

Forum

XS
SM
MD
LG