Ripoti hiyo inasema kwamba tishio kubwa kwa utawala wa Taliban ni kundi la Islamic state na mamluki waliokuwa wanawashambulia maafisa wa usalama wa serikali ya Afghanistan iliyoondoka madarakani.
Ripoti hiyo ambayo imewasilishwa kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa, vile vile inaonya kwamba huenda mashambulizi yakaongezeka wakati wa hali nzuri ya hewa, kati ya wapiganaji wa kundi la Islamic state na Taliban.
Viongozi wa Taliban wameteua watu 41 katika baraza lake la mawaziri na nafasi nyingine serikalini, waliowekewa vikwazo na umoja wa mataifa