Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 22, 2024 Local time: 22:30

Kundi la M23 lauteka mji wa Kalembe mashariki mwa nchi

Waasi wa kundi la M23 wakilinda eneo wakati wa mkutano kati ya maafisa wa Kikosi cha Afrika Mashariki (EACRF) na waasi wa M23 katika kambi ya Rumangabo huko DRC Januari 6, 2023. Picha na Guerchom Ndebo/AFP

Kundi la waasi la M23 limeuteka mji wa Kalembe mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kupanua wigo wake katika eneo hilo, afisa mmoja na mbunge wa zamani walisema Jumatatu.

Kundi la waasi la M23 limeuteka mji wa Kalembe mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kupanua wigo wake katika eneo hilo, afisa mmoja na mbunge wa zamani walisema Jumatatu.

Kundi la M23 linaloongozwa na Watutsi limekuwa likiendesha uasi katika taifa la Afrika ya kati lililokumbwa na ghasia tangu mwaka 2022. Congo na Umoja wa Mataifa zinaishutumu nchi jirani ya Rwanda kwa kuliunga mkono kundi hilo kwa wanajeshi wake na silaha. Rwanda inakanusha hili lakini inasema imechukua kinachojulikana kama hatua za kujihami.

Waasi walikuwa wamekaa kilomita 10 kutoka Kalembe kwa takriban miezi minane kabla ya kuuteka mji huo siku ya Jumapili asubuhi kutoka kwa wanajeshi wa Congo na Wazalendo muungano wa makundi yenye silaha yanayoiunga mkono serikali, Kabaki Alimasi, afisa kutoka eneo la Walikale ambako Kalembe ipo aliiambia Reuters.

Jeshi la Congo halikujibu mara moja ombi la kutoa maoni.

Forum

XS
SM
MD
LG