Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 15:42

Kundi la G7 laahidi kuendelea kuitenga Russia kiuchumi na kisiasa


Mawaziri wa Mambo ya Nje wa kundi la G7
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa kundi la G7

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa kundi la G7 waliahidi Jumamosi kuimarisha kuitenga Russia kiuchumi na kisiasa, wataendelea kupeleka silaha  kwa Ukraine na kukabiliana na  kile kilichoelezwa na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani kama ni “vita ya ngano” vilivyoanzishwa  na Moscow.

Baada ya kukutana katika kasri ya kifahari ya zaidi ya miaka 400 katika mji wa mapumziko katika bahari ya Baltic ya mji wa Weissenhaus, wanadiplomasia waandamizi kutoka Uingereza, Canada, Ujerumani, Ufaransa, Italia, Japan, Marekani na Umoja wa Ulaya pia waliahidi kuendelea kutoa misaada ya kijeshi na kiulinzi kwa Ukraine kwa kadiri “itakavyo kuwa ni muhimu kufanya hivyo.”

Pia watakabiliana na kile walichokiita ni upotoshaji wa habari unaofanywa na Russia kwa lengo la kuzilaumu nchi za Magharibi kuhusiana na masuala ya usambazaji wa chakula duniani kwa sababu ya vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa dhidi ya Moscow na kuisihi China kutoisaidia Moscow au kuhalalisha uvamizi wa Russia, kulingana na taarifa ya pamoja iliyotolewa.

“Je tumefanya vya kutosha kupunguza madhara yaliyoletwa na vita hivi? Siyo vita vyetu. Ni vita vya Rais wa Russia, lakini sisi tunajukumu la kimataifa, “Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock aliwaambia waandishi wakati wa mkutano wa mwisho wa wana habari.

La msingi ni kuongeza shinikizo kwa Russia ni kwa kupiga marufuku au kusitisha kununua mafuta ya Russia huku matarajio ya nchi wanachama wa EU wiki ijayo ni kufikia makubaliano juu ya suala hilo hata kama katika hatua hii iliyofikiwa itabakia kuwa linapingwa na Hungary.

“Tutaharakisha juhudi zetu kupunguza na kuhitimisha utegemezi wa nishati inayosambazwa na Russia na kwa haraka iwezekanavyo, tutaimarisha ahadi ya nchi za G7 kusitisha au kuweka marufuku ya kuagiza makaa ya m awe na mafuta ya Russia,” taarifa hiyo ilisema.

XS
SM
MD
LG