Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:26

Korea yafanya majaribio ya silaha baada ya Biden kuondoka Asia


Watu wa Korea kusini watazama jaribio la silaha kwenye televisheni, Jumatano.
Watu wa Korea kusini watazama jaribio la silaha kwenye televisheni, Jumatano.

Korea kusini imesema kwamba Korea Kaskazini Jumatano imefanyia majaribio makombora matatu ya masafa marefu saa chache baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kukamilisha ziara yake Kaskazini Mashariki mwa Asia.

Maafisa wa Marekani walikuwa wameonya mara kwa mara kwamba Korea Kaskazini inaweza kurusha kombora la masafa marefu, au hata jaribio la nyuklia, wakati au karibu na safari ya Biden barani humo. Wakati Korea Kaskazini ikijiepusha na majaribio yoyote wakati wa ziara ya Biden, uzinduzi wake ulikuja saa 12 tu baada ya kuondoka Japan.

Kombora la kwanza, ambalo huenda ni ICBM, liliruka kwa takriban kilomita 360 na kufikia mwinuko wa kilomita 540, jeshi la Korea Kusini lilisema. Kaskazini pia ilirusha kombora ambalo lilifeli muda mfupi baada ya kuruka pamoja na kombora la tatu la masafa marefu ambalo lilidhaniwa kuwa la masafa mafupi, taarifa zimeongeza.

XS
SM
MD
LG