Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:13

Korea kusini kusitisha makubaliano ya kijeshi na Korea kaskazini


Baadhi ya takataka ambazo Korea kaskazini ilituma Korea kusini May 29 2024
Baadhi ya takataka ambazo Korea kaskazini ilituma Korea kusini May 29 2024

Korea kusini itasitisha makubaliano ya kijeshi ya kupunguza uhasama kati yake na Korea kaskazini, ya mwaka 2018, baada ya Korea kaskazini kurusha maputo yaliyojaa takataka hadi upande wa kusini.

Seoul ilisitisha makubaliano hayo kwa muda hapo mwaka uliopita baada ya Korea kaskazinikutuma kwa anga ya Korea kusini kifaa cha ujasusi.

Korea kusini imesema kwamba itasitisha makubaliano yote ya kijeshi ya September 19 hadi uaminifu utarudi kati ya nchi hizo mbili.

Korea kaskazini ilirusha karibu maputo 1000 yaliyojaa uchafu ikiwemo mabaki ya sigara na vitu vilivyoonekana kama mmbolea upande wa kusini ikishutumu Korea kusini kwa kueneza habari za uongo kupitia maputo dhidi yake.

Korea kusini imetaja hatua hiyo ya jirani wake kuwa kitendo kisico na busara na na kikuiki vikwazo vya umoja wa mataifa dhidi ya Korea Kaskazini.

Forum

XS
SM
MD
LG