Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 06, 2024 Local time: 10:21

Korea Kusini kuanza tena shughuli za kijeshi kwenye mpaka wake na Korea Kaskazini


Ndege ya kivita ya Korea Kusini aina ya U.S.F-16. Picha ya maktaba.
Ndege ya kivita ya Korea Kusini aina ya U.S.F-16. Picha ya maktaba.

Maafisa wa wa Ulinzi wa Korea Kusini wamesema Jumanne kwamba taifa hilo limesitisha kabisa makubaliano yaliyolenga kupunguza mivutano kati yake na Korea Kaskazini, ili kuiruhusu Seoul kuanza tena harakati za kijeshi kwenye mpaka wa Korea.

Uamuzi huo ulioidhinishwa na rais wa Korea Kusini, Yoon Suk Yeol, ni sehemu ya majibu ya Seoul, baada ya Pyongyang kurusha maputo yaliyojaa taka taka na kinyesi upande wa Korea Kusini. Uamuzi huo sasa unatoa nafasi kwa Korea Kusini, kuanza tena mazoezi ya kijeshi yakihusisha silaha za moto, kwenye mpaka na karibu na visiwa vya mstari wa mbele vilivyoko karibu.

Pia unaliruhusu taifa hilo kuanza kutumia vipaza sauti vya propaganda kuelekea Korea Kaskazini. Korea Kaskazini ilisema kuwa ilirusha maputo hayo baada ya mwanaharakati mashuhuri wa haki za binadamu wa Korea Kusini kurusha maputo yaliyokuwa yamejazwa makaratasi yenye maneno ya kuipinga Korea Kaskazini.

Jeshi la Korea Kusini, lilisema kuwa lilipata maputo karibu 1,000 yenye uchafu, yaliyotumwa kwa awamu mbili kutoka Kaskazini. Imeongeza kusema pia kwamba Korea Kaskazini imekuwa ikivuruga mawasiliano ya GPS kwenye eneo la mpakani. Kupitia taarifa ya Jumanne, jeshi la Korea Kusini limesema kuwa vitendo vya Korea Kaskazini vinahatarisha “usalama wa watu wetu,”na kwamba litafanya kila liwezalo kuzuia uchokozi katika siku za zijazo.

Forum

XS
SM
MD
LG