Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 19:32

Korea Kaskazini yajigamba jaribio la Scud linamafanikio


Kiongozi wa Korea Kaskazini akifurahia jaribio la kombora lililotumia teknolojia ya ufanisi mkubwa
Kiongozi wa Korea Kaskazini akifurahia jaribio la kombora lililotumia teknolojia ya ufanisi mkubwa

Shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini limesema jaribio la hivi karibuni la kombora la balistika lilikuwa la mafanikio na limeweza kutumia mtambo wa kongoza kombora hilo ulioweza kulielekeza kwa ufanisi mkubwa.

Katika nchi jirani ya Korea Kusini, Jeshi limesema Jaribio hilo la Jumatatu lilihusisha aina ya kombora la Scud ambalo lilitua kilometa 450 nje ya mwambao wa mashariki ya Korea Kaskazini katika pwani ya Japan.

Jaribio hili, la tatu katika wiki kadhaa, limekuja siku chache baada ya viongozi waliokutana katika mkutano wa kiuchumi wa G7 kushinikiza Pyongyang kuacha utashi wake wa kuwa na silaha za nyuklia.

Shirika la Habari la Korea Kaskazini, KRT, ilitangaza kurushwa kwa kombora hilo siku ya Jumanne katika matangazo yake.

“Jaribio hili la kombora lilikuwa na azma ya kuhakikisha upande wa kiufundi wa kombora hili jipya wenye uwezo wa kulielekeza kwa ufanisi zaidi, na kuliwezesha kupiga eneo la adui bila ya kukosa katika eneo lolote.

Jaribio hilo pia lilikuwa linaangalia uwezo wa kutumia mashine aina ya caterpillar itakayoweza kurusha kombora hilo kutoka kwenye kitako chake cha kwenye gari hilo ambalo limetengenezwa mahsusi na kuundwa kukabiliana na hali mbalimbali za kivita.

Kikosi cha Pacific Command cha jeshi la Marekani kimesema kimeweza kufuatilia na kuona kuwa hilo kombora la balistiki ni la masafa mafupi la dakika sita na kujua kuwa sio tishio kwa Amerika ya Kaskazini.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwenye Twitter, “ Korea Kaskazini imeonyesha dharau ya hali ya juu kwa majirani zake, China, kwa kupiga kwa mara nyingine kombora la balistika.” Lakini Trump amewapa sifa China kwa “Juhudi kubwa” za kujaribu kuidhibiti Korea Kaskazini yenye utashi wa kijeshi.

China imerejea kusema kuwa inaona mazungumzo ndiyo njia ya kutatua mgogoro huu juu programu ya Korea Kaskazini ya nyuklia.

XS
SM
MD
LG