Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 29, 2024 Local time: 02:00

Korea Kaskazini yafanya jaribio la kombora bila mafanikio


Hatua ya Korea Kaskazini kurusha kombora lisilojulikana la masafa marefu kuelekea baharini katika pwani ya mashariki ya Peninsula ya Korea imeonekana kutofanikiwa, jeshi la Korea Kusini limesema Jumatano.

Korea Kaskazini mapema wiki hii ilikosoa kutumwa kwa shehena ya ndege ya Marekani kujiunga na mazoezi ya pamoja na Korea Kusini na Japan, na kuonya kuhusu maonyesho makubwa na mapya ya ulinzi.

Urushaji wa kombora ambalo halikufanikiwa ulitokea karibu na Pyongyang, wanadhimu wa jeshi la Korea Kusini wamesema.

Kikosi cha ulinzi wa pwani cha Japan kimesema kombora linaloaminika kuwa la masafa marefu la Korea Kaskazini limeonekana likianguka.

Wizara ya Ulinzi ya Japan imesema kuwa kombora hilo liliruka juu kwa takriban kilomita 100 na masafa ya zaidi ya kilomita 200 na kusema lilionekana kutofanikiwa.

Forum

XS
SM
MD
LG