Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:12

Korea kaskazini imerusha makombora na kuonya Marekani


Rais wa Korea kaskazini Kim Jong Un akitoa maelezo kwa maafisa wa ngazi ya juu wa jeshi la nchi hiyo April 1, 2015
Rais wa Korea kaskazini Kim Jong Un akitoa maelezo kwa maafisa wa ngazi ya juu wa jeshi la nchi hiyo April 1, 2015

Korea Kaskazini imerusha makombora ya masafa mafupi kuelekea baharini, mashariki mwa nchi hiyo, saa chache baada ya kutishia kuanzisha kile imekitaja kama majibu makali ya kijeshi kutokana na hatua ya Marekani kuimarisha msaada wake wa kijeshi kwa Korea Kusini na Japan.

Makombora hayo yamerushwa kutoka pwani ya Wonsan, Korea Kaskazini, asubuhi, saa tano kasoro dakika 12, kwa saa za Korea Kaskazini.

Yameanguka katika bahari kati kati ya Peninsula ya Korea na Japan.

Majeshi ya Korea Kusini, Marekani na Japan yameshutumu hatua hiyo ya Korea kaskazini na kuonya kwamba inatishia hali ya amani ya eneo hilo.

Hii ni mara ya kwanza katika muda wa siku nane, Korea Kaskazini imefyatua makombora, baada ya mwezi mzima wa kurusha makombora kadhaa yakiwemo ya masafa marefu.

Wataalam wamesema kwamba Korea kaskazini ina mipango ya kuongeza utengenezaji wa silaha za Nyuklia, kwa kiwango kinachokaribia cha mataifa ya magharibi na washindani wake.

XS
SM
MD
LG