Zaidi ya mipira ya Kondomu 17,076 imeondolewa sokoni mara moja kwa kuzingatia ushauri wa mamlaka ya vifaa vya tiba nchini Tanzania TMDA.
“Kondomu ambazo hazikithi ubora unaostahili zimeondolewa madukani," alisema mkurugenzi wa vifaa vya matibabu nchini Tanzania Akida Khea wakati alikuwa akihutubia kikao cha kamati ya TMDA mjini Morogoro, Tanzania.
Khea alisema kwamba kondomu hizo ziliingia Tanzania kwa njia ya magendo na kuwaweka watumiaji katika hatari ya kuambukizwa virusi vya Ukimwi.
Mwaka wa 2019 shirika la Marie stopes liliagiza kuondolewa zaidi ya kondomu milioni moja kutoka madukani nchini Uganda baada ya kugunduliwa kwamba mipira hiyo ilikuwa haikithi viwango na haifai kutumika kabisa.
Kulingana na mamlaka ya dawa nchini Uganda - NDA - Vipimo vya maabara vilibaini kwamba kondomu za Life Guard zilikuwa na mashimo na rahisi kupasuka wakati wa tendo la ngono.