Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 05:15

Kombora la Russia limeshambulia biashara binafsi Ukraine


Kombora la Russia limeshambulia biashara binafsi katika mkoa wa kati wa Ukraine, Vinnytsia, nyakati za usiku, na kujeruhi watu watatu kwa mujibu wa taarifa za serekali ya Ukraine, Ijumaa.

Katika chapisho kwenye Telegram, Gavana Serhiy Borzov, amesema kwamba kuna walioathirika ambao ni raia watatu, na wamepatiwa misaada inayohitajika, ambapo pia aliongeza kwamba magari na mali nyingine zimeharibiwa.

Wakati huohuo, ndege isiyo na rubani ya Ukraine imeshambulia mji mmoja mapema leo magharibi mwa Russia ambapo ni kituo cha moja ya vinu vikubwa vya nyuklia nchini humo.

Maafisa wa Russia wanasema hakuna taarifa za uharibifu katika kinu hicho kilichopo katika mji wa Kurchatov, lakini jengo moja limeharibiwa.

Forum

XS
SM
MD
LG