Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 21:36

Kombora la Russia lashambulia jengo na kuuwa watu watatu


Serekali ya Ukraine, Alhamisi imesema kuwa kombora la Russia lilishambulia jengo la makazi  katika mji wa Zaporizhzhia kusini mwa Ukraine, na kuua takriban watu watatu.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy alitoa taarifa kwenye Telegram kwamba kombora hilo liliharibu jengo la ghorofa tatu, na kwamba juhudi za uokozi zinaendelea.

Alisema taifa la kigaidi linataka kugeuza kila siku ya watu wa Ukraine kuwa ya vitisho. Lakini uovu hautatawala katika nchi, alimalizia kusema rais Zelenskyy.

Jeshi la Ukraine liliripoti Alhamisi kwamba vikosi vya Russia vinaendelea kusonga mbele na kuuvamia mji wa Bakhmut, ambao umekuwa eneo la mapigano makali kwa miezi kadhaa.

XS
SM
MD
LG