Utabiri ulikuwa unaipa matumaini Ujerumani ambayo ina rekodi kubwa katika mashindano ya kombe la dunia kwa kuwa mshindi wa kombe hilo mara nne, lakini wachezaji Ritsu Doan na Takuma Asano wamezima matumaini hayo.
Hadi dakika ya 74, Ujerumani ilikuwa ikiongoza kwa bao 1, lakini Doan amefunga bao la kusawazisha katika dakika ya 75 kabla ya mchezaji mwenzake Asano kuonyesha udhibiti mzuri kwa kufunga bao la ushindi dakika ya 83 na kusababisha furaha kubwa na shangwe kwa mashabiki wa Japan.
Bao la Ujerumani lilifungwa dakika ya 33 na mchezaji Guendogan kwa mkwaju wa penalti.